• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Marekani lapitisha muswada wa mageuzi katika jeshi la polisi kwa kufuata msimamo wa chama

    (GMT+08:00) 2020-06-26 16:46:23

    Bunge la Marekani linaloongozwa na chama cha Democrats limepitisha muswada wa sheria ya mageuzi katika jeshi la polisi kufuatana na msimamo wa chama.

    Muswada huo umepitishwa jana kwa kura 236 za ndio dhidi ya 181 za hapana, huku wabunge watatu wa chama cha Republican wakiungana na upande wa Democrats.

    Chini ya kanuni za bunge hilo, hati zinazoruhusu kukaba na kupiga watuhumiwa zitazuiwa kwa majeshi yote ya usalama, na Idara ya kitaifa ya kushughulikia vitendo vya kimabavu vya polisi itaundwa na kusimamiwa na Wizara ya Sheria.

    Muswada huo, ulioitwa "Muswada wa George Floyd kuhusu Polisi 2020" umepewa jina hilo kutokana na mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd aliyeuawa akiwa chini ya ulinzi wa polisi mjini Minnesota mwishoni mwa mwezi Mei.

    Kifo chake kilisababisha wimbi la maandamano na vurugu katika miji 140 nchini Marekani, huku waandamanaji wakipinga matumizi ya nguvu ya polisi na ubaguzi wa rangi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako