• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CDC Marekani yasema kesi za virusi vya Corona nchini humo zinaweza kuwa mara kumi zaidi ya inavyoripotiwa

    (GMT+08:00) 2020-06-26 16:46:52

    Mkuu wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) Robert Redfield amesema, idadi ya watu waliopata maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo inaweza kuwa mara 10 zaidi ya kesi milioni 2.4 zilizothibitishwa kuwa na virusi hivyo.

    Akizungumza na wanahabari, mkuu huyo amesema makadirio hayo yanatokana na vipimo vya kingamwili, na yanaashiria kuwa takriban Wamarekani milioni 24 wameambukizwa virusi hivyo mpaka sasa. Pia amesema, anaamini kuwa, mpaka sasa, asilimia 5 hadi 8 ya idadi ya watu wako hatarini.

    Kwa mujibu takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha John Hopkins, mpaka kufikia jumanne usiku, zaidi ya kesi milioni 4,400 za virusi vya Corona zimeripotiwa nchini Marekani, huku idadi ya vifo ikizidi 124,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako