• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya 127 ya biashara ya kimataifa yafungwa mjini Guangzhou

    (GMT+08:00) 2020-06-26 17:10:14

    Maonesho ya 127 ya biashara ya kimataifa ya China yaliyofanyika mjini Guangzhou, yamefungwa Jumatano wiki hii.

    Msemaji wa maonesho hayo ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa Kituo cha biashara ya kimataifa ya China Bw. Xu Bing ameeleza kuwa, maonesho hayo yaliyofanyika kwa mara ya kwanza kupitia mtandao wa Internet yalifanyika kwa utulivu, na kushirikisha wateja kutoka nchi na sehemu 217 duniani, na kuweka rekodi mpya katika historia ya maonesho hayo. Wakati huo huo, idadi ya wateja wa ndani pia iliongezeka kwa kiasi kikubwa.

    Maonesho hayo yalifanyika kwa siku kumi kupitia mtandao wa Internet, ambapo kampuni elfu 26 kutoka ndani na nje ya China zilishiriki, bidhaa milioni 1.8 zilioneshwa, na maelfu ya studio zilitangaza maonesho hayo kupitia mtandao wa Internet, na kuingiza msukumo mpya katika biashara ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako