• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaweka zuio katika baadhi ya sehemu mjini Kigali

    (GMT+08:00) 2020-06-26 19:06:16

    Wizara ya Serikali za Mitaa ya Rwanda imewataka wakazi wa baadhi ya sehemu za mji mkuu wa nchi hiyo, Kigali kukaa nyumbani kwa siku 15 kuanzia Alhamisi jioni ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona katika mji huo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inasema, wakazi wanaohusika katika uamuzi huo uliochukuliwa kufuatia tathmini ya afya wanatoka katika wilaya sita. Wale wanaotaka huduma za afya na wenye sababu za dharura tu wanaruhusiwa kutoka, wafanyakazi wa serikali na taasisi za binafsi katika sehemu hizo wanatakiwa kufanya kazi wakiwa nyumbani.

    Wizara hiyo pia imeonya kuwa hatua za zuio huenda zitarejea tena katika sehemu nyingine za Kigali kama tathmini ya afya itaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako