• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona barani Afrika imezidi laki 3

    (GMT+08:00) 2020-06-26 19:30:16

    Takwimu kutoka Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa barani Afrika zimeonesha kuwa, kesi zilizothibitishwa kuwa na virusi vya Corona barani humo zimefikia 336,019, idadi ya vifo imefikia 8,856, wengine 160,833 wamepona.

    Afrika Kusini inaendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya kesi za virusi hivyo, ambapo kesi mpya 6,579 zilithibitishwa jana, kiasi ambacho kimeweka rekodi mpya katika historia yake, na kufanya idadi ya jumla ya maambukizi nchini humo kufikia 118,375, huku waltu waliofariki wakifikia 2,292. Serikali ya nchi hiyo imeamua kujenga kituo kikubwa cha kuhifadhia maiti mjini Cape Town.

    Ethiopia hivi karibuni imeanzisha kampeni ya upimaji wa kingamwili ya virusi vya Corona nchini humo. Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya afya ya umma ya nchi hiyo imesema, shughuli za upimaji zitaendelea hadi tarehe 14 Julai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako