• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona barani Ulaya waongezeka kidogo

    (GMT+08:00) 2020-06-26 19:33:17

    Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika la Afya Duniani barani Ulaya Bw. Hans Kluge amesema, mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona barani humo umeongezeka kidogo kutokana na kulegeza zaidi udhibiti wa jamii wa nchi mbalimbali za Ulaya.

    Bw. Kluge amesema, katika siku za karibuni, Ulaya imeripoti kesi elfu 20 mpya kwa siku na vifo 700, na kuongeza kuwa, kuanzia wiki iliyopita, idadi ya ongezeko la kesi mpya za COVID-19 kwa wiki imeanza kuongezeka. Ameonya kuwa, mfumo wa afya wa baadhi ya nchi za Ulaya utakumbwa na matatizo zaidi kama hazitaimarisha udhibiti.

    Bw. Kluge pia amesema, ingawa vifaa vya kidijitali ni njia yenye ufanisi katika kupambana na maambukizi hayo, lakini amezishauri idara husika za nchi mbalimbali kutumia vifaa hivyo kwa busara ili kutatua suala la usalama wa faragha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako