• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yafuatilia mpango wa Marekani wa kutuma jeshi lake barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-06-26 19:33:56

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Alexsander Grushko amesema, nchi hiyo itafuatilia mpango wa Marekani wa kutuma jeshi lake barani Ulaya na kuchukua hatua za lazima kuhakikisha usalama wa taifa na maslahi ya haki ya Russia kama inahitajika.

    Bw. Grushko amesema, Marekani inaendelea kuharibu msingi wa usalama wa kijeshi wa Ulaya, kujitoa kwenye makubaliano ya kuangamiza makombora ya masafa ya kati na Mkataba wa Anga ya Wazi. Pia amesema Marekani imezuia kuidhinisha marekebisho ya makubaliano ya silaha ya kawaida barani Ulaya, na huenda ikaharibu nyaraka za msingi za uhusiano kati ya Russia na NATO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako