• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya kufungulia mpaka kwa masharti Julai mosi

    (GMT+08:00) 2020-06-28 16:53:37

    Vyombo vya habari vya Ufaransa vilinukuu habari kutoka kwa asasi za kidiplomasia ikisema, Umoja wa Ulaya umeamua kuanzia Julai mosi utafungua mpaka kwa masharti na nchi na sehemu 15 duniani, na Marekani haipo kwenye orodha hiyo kutokana na hali isiyoridhika ya udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Imefahamika kuwa kwenye orodha hiyo ambayo haijatangazwa rasmi, nchi za Afrika ni pamoja na Rwanda, Algeria, Tunisia na Morocco, na nyingine ni China, Japan, Korea Kusini, Thailand, Australia, Serbia, Montenegro, Georgia, New Zealand, Uruguay na Canada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako