• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China yaanza mkutano wake

    (GMT+08:00) 2020-06-29 09:10:02

    Kamati ya Kudumu ya Bunge la 13 la Umma la China imeanza mkutano wake wa 20 jana chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Li Zhanshu, na inatazamiwa kupitia miswada mbalimbali, ukiwemo muswada wa kulinda usalam wa taifa huko Hong Kong.

    Wajumbe wa Kamati hiyo walisikiliza ripoti ya majadiliano ya muswada huo unaohusu kulinda usalama wa taifa katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong nchini China iliyowasilishwa na makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Bw. Shen Chunyao.

    Miswada iliyowasilishwa mbele ya Kamati hiyo ni pamoja na muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Watoto ambao umesomwa kwa mara ya pili na kupendekeza kupunguza mzigo wa kazi za shule kwa wanafunzi, kuhakikisha usalama katika maeneo ya shule na kuzungumzia suala la uonevu shuleni.

    Pia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba Hu Keming alifafanua kuhusu muswada wa sheria wa udhibiti wa usafirishaji wa bidhaa, ambayo imeeleza kwa kina majukumu na mamlaka ya kisheria ya forodha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako