• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi za maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika yazidi laki 3.7

    (GMT+08:00) 2020-06-29 09:17:00

    Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimesema, hadi kufikia Jumapili asubuhi, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona (COVID-19) barani Afrika imefikia 371,548, na idadi ya vifo kutokana na janga hilo imefikia 9,484.

    Kituo hicho kimesema, kanda ya kusini mwa Afrika sasa ni eneo linaloathiriwa zaidi na COVID-19 barani humo.

    Ijumaa iliyopita, Mkurugenzi wa kituo cha Afrika CDC Bw. John Nkengasong alilihimiza bara hilo kujiandaa ongezeko la idadi ya maambukizi ya virusi hivyo baada ya kupunguza hatua za vizuizi. Amesisitiza kuwa ingawa janga hilo limechelewa kutokea barani Afrika, lakini idadi ya kesi za janga hilo na vifo inaongezeka kwa kasi kila siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako