• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msumbiji yaongeza kwa mara ya tatu muda wa hali ya dharura kwa siku nyingine 30

    (GMT+08:00) 2020-06-29 18:15:58

    Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi Jumapili alitangaza kuongeza kwa mara ya tatu muda wa hali ya dharura utakaodumu kwa siku nyingine 30, huku baadhi ya hatua zikilegezwa katika kutafuta hali mpya ya kupambana na janga la COVID-19.

    Kwenye taarifa yake kwa njia ya televisheni, rais Nyusi amesema wameamua kuimarisha hatua ya ngazi ya tatu na kurekebisha baadhi ya hatua ambazo zinaleta athari nchini kwenye utaratibu wa ngazi na kuruhusu sekta kadhaa kuanza shughuli zake.

    Katika kipindi cha kuongeza muda wa hali ya dharura kinachoanza Jumanne, utaratibu wa kulegeza hatua kali utafanyika hatua kwa hatua, na unaweza kubadilishwa kutegemea na hali ya virusi vya Corona. Aidha ametaja kufungua tena kwa baadhi ya sekta zikiwemo elimu, biashara, utamaduni na utalii ambazo amesema lazima zifunguliwe kwa kuzingatia utaratibu mkali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako