• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wamarekani wanaosoma habari kwenye vyombo vya habari vinavyoshikilia ukale wapotoshwa kirahisi zaidi

    (GMT+08:00) 2020-06-29 18:16:54

    Gazeti la The Washington Post la Marekani hivi karibuni limetoa makala ikisema, Wamarekani wanaosoma habari kwenye vyombo tofauti vya habari wana mawazo tofauti kuhusu janga la COVID-19.

    Hojaji zilizofanywa na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania pamoja na Chuo Kikuu cha Illinois kwa watu 1,008 zinaonesha kuwa, watu wanaosoma habari kwenye vyombo vikuu vya habari wana mawazo sahihi zaidi kuhusu virusi vya Corona, huku wale wanaopata habari kutoka kwenye vyombo vya habari vinavyoshikilia ukale wakiamini kirahisi zaidi habari za uongo, kwa mfano Vitamins C inaweza kukinga virusi vya Corona.

    Tasnifu iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi ya Marekani inasema, mawazo yasiyo sahihi kutoka vyombo vya habari yanaweza kuathiri vitendo vya watu katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona. utafiti unaonesha kuwa, watazamaji wa Televisheni ya FOX wakiongezeka kwa asilimia 10, watu wanaofuata agizo la kujitenga nyumbani wanapungua kwa asilimia 1.3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako