• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini chaunga mkono msimamo wa China katika suala la Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-06-29 18:32:12

    Naibu mkurugenzi mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini Bw. Solly Mapaila hivi karibuni alipohojiwa na waandishi wa habari alisema, chama hicho kinaunga mkono sera ya kuwepo kwa China moja duniani, na msimamo wa serikali ya China kuhusu suala la mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong, na kupinga njama yoyote ya kuifarakanisha China. Chama hicho kililaani nchi kadhaa za magharibi kwa kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

    Akisema,"Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini kinaunga mkono sera ya kuwepo kwa China moja, na kupinga kitendo chochote cha kuifarakanisha China na kuharibu umoja wa China. Kama tunavyojua, Uingereza iliitawala Hongkong. Baada ya mkoa wa Hong Kong kurudi China, iliendelea kwa kasi, na makampuni mengi ya nchi za magharibi yalipata maslahi makubwa kwa kufanya biashara kaitka mkoa huo. Lakini nchi kadhaa za magharibi zinajaribu kuharibu utulivu wa Hong Kong, na idara zao huko Hong Kong zilikiuka sheria ya mkoa huo, zikiwalinda na kuwasaidia watu waliofanya ufarakanishaji, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, na vitendo hivyo haviwezi kukubaliwa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako