• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Takriban raia 25 wameuawa au kujeruhiwa kwa makombora kusini mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2020-06-29 18:46:30

    Takriban raia 25 wameuawa au kujeruhiwa leo baada ya makombora kushambulia soko la wilaya ya Sangin lililopo mkoa wa Helmund kusini mwa Afghanistan.

    Kwa mujibu wa chanzo cha habari, polisi wameanza kufanya uchunguzi wa shambulizi hilo lililotokea nyakati za saa 3:30 asubuhi ili kujua aliyerusha kombora hilo. Taarifa za awali zilisema takriban watu 10 waliuawa, na majeruji wamekimbizwa kwenye hospitali kuu ya upasuaji katika mji mkuu wa jimbo Lashkar Gah. Kwa mujibu wa wanakijiji shambulizi hilo lilitokea wakati wa mapambano makali kati ya wapiganaji wa Taliban na vikosi vya usalama vya serikali kwenye soko la wilaya.

    Msemaji wa Taliban, Zabiullah Mujahid amewaambia wanahabari kuwa kombora lilirushwa na Jeshi la Taifa la Afghanistan, lakini msemaji wa serikali ya mkoa Omar Zwak amesema taarifa zaidi zitatolewa kwa vyombo vya habari baadaye leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako