• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyibiashara wanaoficha mafuta kupigwa faini.

    (GMT+08:00) 2020-06-29 19:12:37

    Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imevifutia leseni za uuzaji wa mafuta vituo vitano, kwa makosa ya kuficha, kutouza na kuuza mafuta juu ya bei elekezi huku ikotoa onyo kali kwa wauzaji wa nishati hiyo wanaojaribu kufanya hujuma na kukiuka maagizo ya Serikali.

    Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Ewura, Titus Kaguo, alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya tathmini ya kina iliyowawezesha kubaini kuwa kuna sababu za makusudi kwa wauzaji hao kuhujumu uuzaji wa mafuta.

    Alisema katika uchunguzi wa awali uliofanywa na Ewura, kuna dalili za wauzaji wa mafuta kufanya hujuma kwa kuwanyima wananchi mafuta kwa makusudi na kutoa onyo kwa waauzaji wote kutofanya hujuma ambazo zitawaingiza katika uhujumu uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako