• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Ethiopia wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2020-06-30 08:46:51

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amezungumza na mwenzake wa Ethiopia Bw. Gedu Andargachew kwa njia ya simu.

    Bw. Wang amesema, China inapenda kushirikiana na Ethiopia na nchi nyingine za Afrika kutekeleza vizuri mafanikio yaliyopatikana katika mkutano maalum wa mshikamano wa China na Afrika katika kupambana na mlipuko wa COVID-19. Amesema China itaendelea kusukuma mbele utekelezaji wa mafanikio yaliyopatikana katika Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta za afya, kuanza mapema ujenzi wa makao makuu ya Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika, na kuharakisha mazungumzo na nchi za Afrika kutekeleza mpango wa kupunguza deni la kundi la G20. Pia amesema, China inasifu Ethiopia kuunga mkono haki ya China katika suala la Hong Kong.

    Kwa upande wake, Bw. Andargachew amesema, mafanikio ya mkutano huo maalum na mkutano wa ngazi ya juu ya ushirikiano wa kimataifa wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kumeonesha China inajitahidi katika ushirikiano wa kupambana na COVID-19. Pia amesema, Ehiopia inaunga mkono sera ya China Moja, na suala la Hong Kong ni mambo ya ndani ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako