• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yachelewesha mapokezi ya wakimbizi wa DRC kutokana na wasiwasi wa suala la usalama

    (GMT+08:00) 2020-06-30 08:58:20

    Uganda jana imesema imechelewa kuwapokea maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaokimbilia nchini humo kutokana na hofu ya kiusalama .

    Waziri anayeshughulikia misaada, majanga na wakimbizi nchini Uganda Bw. Hilary Onek amesema uamuzi huo umekuja baada ya tukio lililotokea mwezi Machi, ambapo baadhi ya wakimbizi kutoka DRC na wananchi wa Uganda walifanya mashambulizi dhidi ya jeshi kwenye mji wa mpaka wa magharibi wa Zombo, na kusababisha vifo vya askari 3 na washambuliaji 17.

    Bw. Onek amesema serikali inataka kuhakikisha kuwa hakuna maadui wanaoingia nchini humo na kufanya mashambulizi kutoka ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako