• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wa Afrika wapendekeza kubadilisha sera ili kuchochea ukuaji baada ya kumalizika mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-30 09:01:39

    Wataalam na watunga sera kutoka bara la Afrika wamezitaka serikali za kanda ya Afrika kusini mwa Sahara kuanza mchakato wa kubadilisha sera ili kuchochea ukuaji kutokana na athari za virusi vya Corona, na pia kuimarisha unyumbufu dhidi ya athari za baadaye.

    Wataalam na watunga sera hao wamesema hayo katika mkutano uliofanyika kwa njia ya video jijini Nairobi, Kenya.

    Mkurugenzi Mtendaji wa jopo la washauri bingwa kutoka Mashirika ya Utafiti wa Uchumi wa Afrika Njuguna Ndung'u amesema, ni lazima kutunga sera zenye mazingira ya uchumi mpana, kulinda uwekezaji wa ndani na kuimarisha maingiliano ya kibiashara katika bara la Afrika.

    Waziri wa Viwanda na Biashara wa Kenya Betty Maina amesema, kuna fursa ya kuanzisha utaratibu mpya baada ya janga la virusi vya Corona ambao utahakikisha kipato kizuri kwa familia, kuchochea uvumbuzi, ushindani na ukuaji.

    Nchi za Afrika zimeathiriwa na mnyororo wa ugavi unaohusishwa na mlipuko wa virusi vya Corona, na uchumi katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara unatarajiwa kushuka kwa asilimia 3.2 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako