• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi wake kutokana na hali ya kaskazini magharibi mwa Syria

    (GMT+08:00) 2020-06-30 09:02:09

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu Mark Lowcock ameeleza wasiwasi wake kutokana na hali ya kaskazini magharibi mwa Syria.

    Bw. Lowcock ameliambia Baraza la Usalama la Umoja huo kuwa, inakadiriwa kuwa watu milioni 2.8 katika eneo hilo wanahitaji msaada wa kibinadamu. Amesema karibu watu milioni moja wamekimbia makazi yao mapema mwaka huu, na hali mbaya ya kiuchumi inayotokana na mlipuko wa virusi vya Corona imewafanya watu katika eneo hilo kuwa moja kati ya watu walio hatarini zaidi nchini Syria.

    Amesema chini ya mfumo wa kusambaza misaada ya kibinadamu kupitia mpakani ulioidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, malori 1,781 yaliyobeba vifaa vya misaada yalivuka mpaka kutokea Uturuki na kuingia kaskazini magharibi mwa Syria mwezi Mei.

    Amesema kiwango cha msaada kinachotolewa sasa kupitia eneo hilo bado ni kidogo, na kinapaswa kuongezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako