• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaomba Interpol kusaidia kumkamata Trump

    (GMT+08:00) 2020-06-30 09:08:35

    Iran imeomba msaada wa Shirika la Polisi wa Kimataifa Interpol kumkamata rais Donald Trump wa Marekani pamoja na maofisa wengine 35 wa kisiasa na kijeshi wa nchi hiyo waliohusika na mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani wa Iran mwezi Januari. Mwendesha mashtaka mkuu wa Iran Ali Qasi Mehr amesema hayo hapo jana, na kuongeza kuwa watu hao 36 kwa jumla wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji na ugaidi. Interpol bado halijajibu habari hiyo. Jenerali Soleimani aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha jeshi la Iran aliuawa na makombora yaliyorushwa na jeshi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako