• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mradi wa "kurejesha mashamba ya kilimo kuwa misitu na mbuga nchini China wachangia uhifadhi wa mazingira duniani

  (GMT+08:00) 2020-06-30 18:22:55

  Idara ya Misitu na Mbuga ya Taifa ya China leo imetoa waraka kuhusu mradi wa kurejesha mashamba ya kilimo kuwa misitu na mbuga ambao umeendelea nchini China kwa miaka 20, na kusema katika miaka 20 iliyopita China iliwekeza zaidi ya dola bilioni 73 za Kimarekani kwa ujumla na kurejesha mashamba hekta bilioni 343.4 kuwa misitu na mbuga, na ongezeko la misitu na mbuga kutokana na mradi huo linachukua asilimia 4 ya ongezeko la eneo la kijani duniani.

  Waraka huo unaonesha hali ya jumla ya utekelezaji wa mradi huo katika miaka 20 iliyopita. Kwa mujibu wa waraka huo, upandaji wa miti kutokana na mradi huo umechukua asilimia 40.5 ya upandaji wote wa miti nchini China, na mazingira yaliboreshwa kidhahiri na kuwanufaisha wakulima milioni 158 moja kwa moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako