• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa mkoa wa Hong Kong akaribisha kupitishwa kwa sheria ya usalama wa taifa ya mkoa huo

    (GMT+08:00) 2020-06-30 20:12:23

    Kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China leo imepitisha Sheria ya Kulinda Usalama wa Taifa ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong wa Jamhuri ya Watu wa China. Mkuu wa mkoa huo bibi Carrie Lam ametoa taarifa ya kuipokea sheria hiyo.

    Kwenye taarifa hiyo bibi Lam amesema Hong Kong ni sehemu isiyotengeka ya China, na kutawaliwa moja kwa moja na serikali kuu, kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa la China ni wajibu wa kisheria wa Hong Kong, na pia kunahusisha wakazi wote wa mkoa huo. Sheria hiyo ni hatua muhimu ya kukamilisha sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", na pia itasaidia jamii ya Hong Kong kurejesha utulivu.

    Bibi Lam amesema, ana imani kuwa baada ya kutekelezwa kwa sheria ya usalama wa taifa, vurugu zilizoukumba mkoa wa Hong Kong zitapungua, na utulivu utarejea. Hong Kong itafunga safari mpya na kushughulikia maendeleo ya uchumi na kuboresha maisha ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako