• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakanusha kauli zisizo sahihi zilizotolewa na mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-07-01 09:08:26

    Taarifa ya Ujumbe wa China kwenye Umoja wa Mataifa imekanusha kauli zisizo sahihi kuhusu China zilizotolewa na balozi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja huo.

    Taarifa hiyo imesema, balozi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa jana alitoa taarifa inayoonesha msimamo wenye upendeleo, kupotosha hali halisi ya haki za binadamu nchini China, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, kauli inayopingwa vikali na China.

    Taarifa hiyo imesema, jamii ya kimataifa inapaswa kufuatilia zaidi haki za binadamu nchini Marekani. Baraza la Haki za Binadamu la Umoja huo lilifanya mjadala wa dharura hivi karibuni na kupitisha kwa kauli moja azimio linalolaani vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyosababisha kifo cha George Floyd.

    Taarifa hiyo pia imesema China ina nia thabiti ya kulinda maslahi ya nchi, na jaribio lolote la kuipaka China matope kwa suala la haki za binadamu halitafanikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako