• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yapitisha bajeti ya dola za kimarekani milioni 300 ili kuiunga mkono Uganda

    (GMT+08:00) 2020-07-01 09:20:11

    Benki ya Dunia imepitisha bajeti ya dola za kimarekani milioni 300 ili kuiunga mkono Uganda kupunguza athari za kiuchumi zinazotokana na janga la COVID-19.

    Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo imesema, bajeti hiyo ni operesheni ya kwanza ya uungaji mkono wa bajeti katika miaka 6 iliyopita, na itatumika kushughulikia pengo la fedha, pia kuunga mkono mageuzi yanayotoa misaada ya moja kwa moja kwa watu binafsi na biashara zilizoathiriwa vibaya zaidi na janga la COVID-19.

    Meneja wa tawi la Benki ya Dunia nchini Uganda Bw. Tony Thompson amesema, operesheni hiyo itawezesha serikali ya Uganda kutoa huduma muhimu, mtandao wa usalama wa jamii, na mfumo madhubuti wa kukabiliana na mshtuko kwa muda mrefu, na kusaidia kasi ya kufufuka kwa uchumi wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako