• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ILO: Hakuna uhakika wa kufufuka kwa soko la nguvukazi duniani

    (GMT+08:00) 2020-07-01 09:20:57

    Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) limesema kutokana na athari za kuenea kwa virusi vya Corona, muda wa kazi umepungua kwa kiasi kikubwa duniani katika nusu ya kwanza mwaka huu, bado hakuna uhakika wa kufufuka kwa soko la nguvukazi katika nusu ya pili mwaka huu, na bado kuna hatari ya watu wengi kukosa ajira. Taarifa iliyotolewa jana na Shirika hilo imesema, muda wa kazi duniani ulipungua kwa asilimia 14 katika miezi mitatu kuanzia Aprili hadi Juni, ambao ni sawa na nafasi milioni 400 za ajira. Taarifa hiyo inaongeza kuwa, wafanyakazi katika nchi zinazoendelea na hususan wanawake ndio wanaoathiriwa vibaya zaidi na janga hilo la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako