• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi 52 zapongeza hatua ya China kupitisha sheria ya usalama wa taifa mkoani Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-07-01 09:31:11

    Nchi 52 zimepongeza hatua ya Bunge la Umma la China ya kupitisha sheria ya ulinzi wa taifa katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong.

    Taarifa iliyosainiwa na nchi hizo na kusomwa na Cuba katika mkutano wa 44 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa imesema, kutoingia mambo ya ndani ya nchi huru ni kanuni muhimu iliyosisitizwa kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na ni msingi wa uhusiano wa kimataifa.

    Taarifa hiyo pia imesema, hatua hiyo itasaidia kuhakikisha sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" inadumishwa, na kwamba Hong Kong itafurahia ustawi na utulivu wa muda mrefu. Aidha, taarifa hiyo imesema kwa kupitia sheria hiyo, haki halali na uhuru wa wakazi wa Hong Kong inaweza kutimizwa katika mazingira salama.

    Wabunge wa China walipitisha sheria hiyo katika mkutano wa 20 wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la 13 la Umma la China Jumanne wiki hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako