• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong yaweza kutuliza mkoa huo

    (GMT+08:00) 2020-07-01 17:26:19

    Naibu mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya Hong Kong na Macao ya baraza la serikali la China Bw. Zhang Xiaoming leo hapa Beijing amesema, sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong inaweza kugeuza hali ya Hong Kong na kupata ufanisi. Kwa ujumla sheria hiyo inaweza kutuliza Hong Kong.

    Katika mkutano na waandishi wa habari wa ofisi ya habari ya baraza la serikali la China kuhusu sheria hiyo, Bw. Zhang Xiaoming ameeleza mambo manne kuhusu umuhimu wa sheria hiyo. Kwanza ni hatua muhimu ya sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili". Kutungwa kwa sheria hiyo ni hatua muhimu zaidi ya serikali kuu ya China katika kutatua suala la Hong Kong, ni sheria muhimu ya pili ya serikali kuu kwa ajili ya Hong Kong. Pili, ni alama mpya ya serikali kuu kukamilisha mkakati wa kutawala Hong Kong. Tatu, ni ulinzi wa utulivu na ustawi wa Hong Kong. Nne, sheria hiyo itageuza hali ya Hong Kong, na kuirudisha kwenye njia sahihi ya kujiendeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako