• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yavitaka vyombo vinne vya habari vya Marekani kutoa taarifa kwa China

    (GMT+08:00) 2020-07-01 17:43:29

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo ametangaza kuwa, ikiwa hatua za kujibu vitendo vya Marekani kukandamiza vyombo vya habari vya China, China inataka shirika la habari la Marekani AP, Shirika la habari la UPI, kampuni ya utangazaji CBS, na kituo cha redio ya umma cha Marekani NPR kuitolea China nyaraka zote za wafanyakazi wao, mambo ya fedha, uendeshaji na umiliki wa mali zisizohamishika nchini China.

    Bw. Zhao amesema, katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Marekani imeweka vizuizi bila msingi wowote kwa vyombo vya habari vya China nchini Marekani na wafanyakazi wake kufanya sughuli za utangazaji wa habari za kawaida, kuongeza zaidi ubaguzi na shinikizo la kisiasa kwa vyombo vya habari vya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako