• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Ukuaji wa uchumi wapungua hadi asilimia 4.9

    (GMT+08:00) 2020-07-01 18:13:09

    Ukuaji wa uchumi wa Kenya umepungua hadi asilimia 4.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu kutoka asilimia 5.5 mwaka jana,ikiwa ni ukuaji wa polepole zaidi katika miaka nane.

    Kulingana na takwimu za Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa ya Kenya (KNBS) huo ulikuwa ukuaji wa polepole wa kwanza tangu mwaka 2012 licha ya kuongezeka kwa jumla kwa mauzo ya nje,

    Kumekuwa na upungufu wa ukuaji wa asilimia 9.3 kwenye sekta utalii na huduma za chakula ikichangiwa na kushuka kwa watalii kutoka ulaya na Marekani kutokana na janga la virusi vya corona.

    Hata hivyo ukuaji umesaidiwa na sekta ya kilimo, ambayo inachukua zaidi ya theluthi moja ya Pato la Taifa (GDP).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako