• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Benki ya Dunia yaidhinisha bajeti ya dola milioni 300 kusaidia Uganda

    (GMT+08:00) 2020-07-01 18:13:30

    Benki ya Dunia imeidhinisha bajeti ya dola milioni 300 kusaidia Uganda katika kupigana na virusi vya corona.

    Benki hiyo imetangaza kuwa pesa hizo zitatumika kuongeza uwezo wa serikali kuzuia, kugundua na kutibu corona, kulinda maskini na wanyonge na kusaidia urejeshaji wa uchumi.

    Ilisema juhudi za Uganda za kuzuia kuenea kwa corona kumeathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo na inaweza kusukuma zaidi ya watu milioni 3.15 katika umaskini.

    Tayari, raia wa Uganda karibu milioni 8.7 wanaishi chini ya safu ya umaskini ya chini ya dola mbili kwa siku.

    Mlipuko wa Covid-19, mafuriko na uvamizi wa nzige umeathiri uchumi na kupunguza kiwango cha ukuaji unaokadiriwa kuwa asilimia chini ya 3-4 katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 kutoka kwa wastani wa asilimia 6.3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako