• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya yajipanga kurejelea uagizaji wa mitumba

    (GMT+08:00) 2020-07-01 18:14:03

    Kenya inajipanga kuunda miongozo itakayoruhusu kuanza tena kuingiza nguo na viatu kuukuu yaani mitumba.

    Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku uagizaji wa mavazi makuukuu ambayo ni sekta inayotegemewa na maelfu ya watu.

    Waziri wa Viwanda na Biashara, Betty Maina amelitaka shirika la Viwango vya bidhaa nchini humo kuangalia uwezekano wa kuondoa marufuku ya mwezi Machi lakini pia kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona.

    Mkurugenzi wa shirika la kukadiria ubora wa bidhaa Bernard Njiraini alisema ufunguaji wa hatua kwa hatua katika nchi za Marerkani, Ulaya na China utawezesha wakaguzi wa Kenya walioko kwenye nchi hizo kuhakiki hatua za usafi.

    Kamati ya ufundi, ambayo ni pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (Kemri) na Mamlaka ya Ugavi wa bidhaa za Matibabu ya Kenya (Kemsa), watatakiwa kuamua ikiwa virusi vya corona vinaweza kudumu kwa muda unachukua meli kutoka kwenye nchi hizo hadi Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako