• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mikoa yatakiwa kutenga maeneo ya uwekezaji

    (GMT+08:00) 2020-07-01 18:14:45

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) wa Tanzania Angellah Kairuki, ameiomba mikoa na halmashauri kutenga maeneo ya uwekezaji na kuyawekea miundombinu stahiki ili kuwavutia wawekezaji.

    Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 5 katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya iliyomsaidia kujifunza, kujionea uwekezaji pamoja na kuzungumza na wawekezaji katika ukanda huo.

    Alikipongeza Kituo cha Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), kwa kuwa mfano mzuri katika kuhamasisha uwekezaji, na kutaka taasisi zingine kuiga mfano huo.

    Waziri alisema mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali zikiwamo za utalii, kilimo na ufugaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako