• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kutotajwa kwenye orodha ya nchi zilizoondolewa zuio la kuingia Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-07-01 18:41:57

    Baraza la Umoja wa Ulaya jana lilipitisha pendekezo la kuondoa zuio la kuingia kwa wakazi wa baadhi ya nchi za tatu kuanzia leo Jumatano, huku Marekani ikiwa haimo kwenye orodha hiyo.

    Baraza limependekeza kuondoa kwa zuio la kusafiri kwa wakazi wa Algeria, Australia, Canada, Georgia, Japan na Montenegro. Nyingine ni New Zealand, Rwanda, Serbia, Korea Kusini, Thailand, Tunisia na Uruguay. Wakazi wa Andorra, Monaco, San Marino na Vatican wanazingatiwa kama wakazi wa Umoja wa Ulaya kulingana na pendekezo hilo.

    Marekani, ambayo kawaida ni mshirika wa EU na ni chanzo muhimu cha utalii, yenyewe haipo kwenye orodha. Mipaka ya nje ya jumuiya hiyo ilifungwa tangu katikati ya Machi kutokana na janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako