• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Syria yakemea mkutano wa Brussels kwa kuuita ni uingiliaji wa mambo ya ndani ya Syria

    (GMT+08:00) 2020-07-01 19:19:39

    Wizara ya mambo ya nje ya Syria leo imekemea mkutano wa Brussels juu ya Syria kwa kuuita ni uingiliaji wa mambo ya ndani ya Syria na misimamo iliyopitishwa kwenye mkutano huo inaonesha muendelezo wa sera kali za Marekani na Umoja wa Ulaya dhidi ya Syria.

    Siku moja nyuma, Mkutano wa IV wa Brussels wa kuunga mkono mustakabali wa Syria ulifanyika na kuongozwa na Umoja wa Ulaya na Marekani. Mabunge ya Ulaya yalikataa kurejesha uhusiano wa kawaida na serikali ya rais Bashar al-Assad.

    Wizara hiyo pia imesema tawala zinazomwaga damu za Wasyria, kuharibu mafanikio yao, kuiba utajiri wao na kuwawekea vikwazo haziwezi kuficha uhalifu wao kwa kisingizio cha ubinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako