• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yaidhinisha mpango wa kuwahamisha wanajeshi 9,500 walioko Ujerumani

    (GMT+08:00) 2020-07-02 09:00:34

    Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, rais wa nchi hiyo Donald Trump ameidhinisha mpango wa kuwahamisha askari 9,500 wa Marekani walioko nchini Ujerumani. Rais Trump alisema anafikiria kupunguza askari wa Marekani nchini Ujerumani kutoka elfu 35 hadi elfu 25 kutokana na kwamba, Ujerumani haijalipa ada za kijeshi za NATO. Amesema askari watakaoondoka Ujerumani watapelekwa nchini Poland, ambayo italipa ada zake. Akijibu kauli hiyo, Chansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel amesema, kama Marekani haitaki kubeba wajibu wa nchi kubwa duniani, Ulaya inapaswa kufanya tathmini tena juu ya uhusiano kati yake na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako