• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza hatua za kujibu kitendo cha Marekani cha kukandamiza vyombo vya habari vya China

    (GMT+08:00) 2020-07-02 09:31:33

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, China imevitaka vyombo vinne vya habari vya Marekani kutoa taarifa kwa maandishi, kuhusu wafanyakazi wake, fedha, operesheni na majengo wanayomiliki nchini China, na taarifa hiyo inatakiwa ndani ya siku saba, ikiwa ni kujibu kitendo vha ukandamizaji kilichofanywa na Marekani dhidi ya vyombo vya habari vya China.

    Zhao amevitaja vyombo hivyo vya habari vya Marekani kuwa ni Associated Press, United Press International, The Columbia Broadcasting System, na National Public Radio.

    Hatua hiyo imekuja ikiwa ni kujibu tangazo lililotolewa Juni 22 na Marekani kuwa, Kituo Kikuu cha Televisheni cha China, magazeti ya People's Daily na The Global Times, na China News Service yamewekwa kwenye ngazi ya majukumu ya kigeni nchini Marekani.

    Pia amesema, kitendo hicho cha Marekani kinatokana na mtazamo wake wa Vita Baridi na upendeleo, na kimeharibu hadhi na taswira ya vyombo vya habari vya China, kuathiri utendaji wao wa kazi nchini Marekani, na kuvuruga mawasiliano ya watu na watu na ya kitamaduni kati ya watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako