• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi 46 zaunga mkono kazi ya China katika kupambana na msimamo mkali na ugaidi mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-07-02 09:31:57

    Nchi 46 zimetangaza kuunga mkono kazi ya China katika kupambana na ugaidi na msimamo mkali katika Mkoa Unaojiendesha wa Xinjiang Uygur.

    Taarifa ya pamoja ya nchi hizo iliyosomwa na mjumbe wa Belarusi wakati wa mkutano wa 44 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa imezitaka pande mbalimbali kujizuia kutoa tuhuma zisizo za kweli dhidi ya China kutokana na taarifa potofu. Nchi hizo zimesisitiza kuwa kazi ya Baraza la Haki za Binadamu inapaswa kufanywa bila upendeleo, kwa uwazi, bila ubaguzi, kiujenzi, na kutohusisha siasa.

    Pia taarifa hiyo imesema, kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali ya China, hakuna shambulizi la kigaidi lililotokea mkoani Xinjiang katika miaka mitatu iliyopita, na utulivu na usalama vimerejeshwa mkoani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako