• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu COVID-19 ni ushindi wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2020-07-02 09:32:32

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun amesema kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu virusi vya Corona ni ushindi wa pande nyingi.

    Balozi Zhang amesema katika wakati huu muhimu ambapo dunia inapambana na virusi vya Corona, Baraza hizo linalazimika kuchukua hatua kukabiliana na athari hasi za virusi hivyo katika amani na usalama wa kimataifa. Kupitishwa kwa azimio hilo namba 2532 kunaonyesha uwezo wa Baraza hilo kuchukua nafasi yake ya uongozi, na kuwakilisha ushindi wa pande nyingi.

    Azimio hilo lililoungwa mkono na nchi 15 wajumbe wa Baraza hilo, linataka kusitishwa mara moja na kwa pande zote vitendo vyote vya chuki katika ajenda zote za Baraza la Usalama. Pia linatoa wito kwa pande zote zinazohusika na mapambano ya kutumia silaha kusimamisha vita kwa sababu za kibinadamu kwa siku 90, ili kuwezesha kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu katika maeneo husika, na pia kuwasaidia watu kupata huduma ya matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako