• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya nje ya Rwanda katika jukwaa la biashara ya mtandaoni la Alibaba yakua kwa asilimia 124

    (GMT+08:00) 2020-07-02 19:27:07

    Mauzo ya nje ya Rwanda kupitia jukwaa za uuzaji na ununuaji bidhaa mitandaoni la Alibaba yameongezeka kwa 124% katika mwaka 2019.

    Haya ni kwa mujibu wa habari kutoka Alibaba.

    Kampuni hiyo kubwa ya China ya uuzaji bidhaa mitandaoni ilifungua milango yake kwa ajili ya bidhaa za Rwanda mwaka 2018 wakati ilipotia saini ya jukwaa la dunia la biashara ya mitandaoni (Ewtp) nan chi hiyo.

    eWTP inalenga kufungua masoko kwa baishara ndogo barani Afrika kushiriki katika biashara za kimipaka mtandaoni.

    Kutokana na mkataba huo,Alibaba imezitambulisha bidhaa za Rwanda kwa wateja wa China mtandaoni,mbali na kutangaza bidhaa za utalii za Rwanda katika nchi ya China.

    Bila shaka kahawa ndio bidhaa ya kipekee kutoka Rwanda inayonunuliwa kwa wingi nchini China,ijapokuwa pilipili pia nayo inafuatia.

    Kuna nembo kadhaa za kahawa ya Rwanda zinazouzwa katika jukwaa la Alibaba la Kimataifa la Tmall.

    Tangu mwaka jana mtandao wa Alibaba umekuwa ukiandaa matamasha ya mtandaoni ya kuitangaza kahawa ya Rwanda kwa walaji wa China.

    Mojawapo ya matamasha hayo lilifanyika mwezi Mei mwaka huu,ambapo tani 1.5 ya kahawa ya Rwanda iliuzwa ndani ya dakika moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako