• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaingia kwenye kundi la nchi zenye kipato cha kati

    (GMT+08:00) 2020-07-02 19:27:28

    Waziri wa fedha na mipango,nchini Tanzania, Dk. Philip Mpango,jana alisema benki ya Dunia imetangaza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi tano duniani zilizoingia kwenye kundi la nchi za kipato cha kati kwa kundi la chini mwaka 2020.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk. Mpango alisema kwa mujibu wa benki hiyo, kigezo muhimu cha kwanza cha kutambua nchi zenye uchumi wa kati ni wastani wa pato la mwananchi la kiwango cha kati ya dola za Marekani 1,036(Sh.Milioni 2.3) hadi dola za Marekani 4,045(Sh.Milioni 9.3) kwa kundi la chini.

    Alisema kwa mujibu wa Benki ya Dunia Tanzania ni miongoni mwa nchi tano zilizoingia kundi la kipato cha kati ambapo nchi nyingine ni Algeria, Sri Lanka, Benin na Nepal.

    Waziri huyo alimshukuru Rais John Magufuli, kwa jitihada kubwa za kukuza uchumi wa nchi na kuiwezesha Tanzania kuingia katika hatua hiyo.

    Aliongeza kuwa hatua hiyo ina manufaa mengi, yakiwemo kuongezeka kwa wigo wa upatikanaji wa fedha za mikopo ya kibiashara kwa ajili ya miradi ya maendeleo, kuwa na uhuru na kupanga matumizi na kuondokana na kadhia ya utegemezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako