• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaanza tena utalii wa mikutano

    (GMT+08:00) 2020-07-02 19:28:16

    Shirika la Mikutano la Rwanda (RCB) jana lilitangaza kufungyliwa upya kwa mikutano na makongamano ,wakati nchi hiyo ikijaribu kufufua sekta za utalii na ukaraimu hatua kwa hatua ,ambazo ni kuu kwa uingizaji wa fedha za kigeni.

    Kutokana na hatua hiyo,RCB imeagiza waandaaji na wamiliki wa kumbi kuweka hatua za kukinga maambukizi.

    RCB ilisema miongozo hiyo inalenga kuimarisha mifumo iliyoko katika sekta ya mikutano,motisha,makongamano na maonyesho-MICE-ili kuhakikisha usalama wa wajumbe.

    Miongozo hiyo pamoja na mengine ni ukaguaji wa washiriki wote,kuzingatia umbali baina ya watu,matumizi ya vifaa vya kujikinga,na mifumo ya vieuzi kwa ajili ya kuosha mikono.

    Shirika la RCB liliongeza kuwa miongozo hiyo itazingatiwa kwa matukio ya kiwango cha aina yoyote.

    Sekta ya mikutano iliipatia Rwanda nafasi ya pili kama kituo pendwa cha mikutano barani Afrika.

    Mwaka 2019,sekta hiyo iliingiza $56 milioni (takriban Rwf53 bilioni), sawa na asilimia 20 ya mapato yote ya utalii..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako