• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaona Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha uamuzi kuhusu COVID-19 ni ushindi wa hali yenye pande nyingi

    (GMT+08:00) 2020-07-02 20:51:33

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo hapa Beijing amesema, China inakaribisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha uamuzi kuhusu COVID-19, hatua hiyo ni matokeo muhimu ya Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama, na ni ushindi wa hali yenye pande nyingi.

    Bw. Zhao amesema, kupitishwa kwa umuzi huo kunaonyesha maoni ya pamoja ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa kwamba wanaunga mkono umuhimu wa umoja huo na mashirika yake na kushirikiana kupambana na virusi vya Corona, kuonyesha utekelezaji, na uongozi wa baraza la usalama.

    Bw. Zhao amesema China inatoa mwito kwa pande mbalimbali kutekeleza wazo la jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, kueneza hali yenye pande nyingi, na kushirikiana kupambana na virusi vya Corona, kulinda lengo na kanuni ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kulinda mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Umoja wa Mataifa. Pia amesisitiza kuwa, China itashirikiana na pande mbalimbali, kutekeleza uamuzi huo, kuunga mkono baraza la usalama kuendelea kufanya kazi yake kwa kufuata wajibu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako