• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya washiriki wa kigeni katika maonesho ya kimataifa ya biashara nchini Tanzania yapungua kutokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-07-03 09:24:53

    Waziri wa viwanda na biashara wa Tanzania Bw. Innocent Bashungwa jana amesema, kutokana na athari ya janga la COVID-19, idadi ya washiriki wa kigeni katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Tanzania (DITF) imepungua hadi 43 kutoka 580 ya mwaka uliopita.

    Bw. Bashungwa amesema, baada ya mlipuko wa COVID-19, nchi nyingi duniani zimechukua hatua za kufunga mipaka na usafiri, jambo lililosababisha kupungua kwa idadi ya washirki wa kigeni katika maonesho hayo.

    Naibu mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa Khamis amesema, wengi wa washiriki 43 wa kigeni wanatoka nchi zinazofanya biashara nchini Tanzania, zikiwemo China, Syria, Misiri, Uturuki na Ufilipino, na maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe Mosi hadi 13 mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako