• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CPPCC yapinga muswada wa Marekani kuhusu Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-07-03 10:08:57

    Kamati ya Mambo ya Kigeni ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) limelalamikia na kupinga vikali hatua ya bnge la Marekani kupitisha "Sheria ya Kujitawala ya Hong Kong".

    Taarifa iliyotolewa na Kamati hiyo imesema, hatua hiyo ya Marekani inaingilia kati mambo ya ndani ya China, na inakinzana na sheria ya kimataifa na kanuni za msingi zinazosimamia uhusiano wa kimataifa.

    Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, usalama wa taifa ni hitaji muhimu la uwepo na maendeleo ya nchi, na inahusika na maslahi makuu ya nchi husika, na kuongeza kuwa hakuna nchi duniani inaweza kufumbia macho hatua na vitendo vinavyokiuka kimsingi usalama wa nchi hiyo.

    Taarifa hiyo pia imesema, utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Usalama wa Taifa katika Mkoa wenye Utawala Maalum wa Hong Kong utasaidia kumaliza vurugu katika mkoa huo na kuanza upya shughuli za maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako