• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Real Madrid yazindua kikosi cha soka ya wanawake

    (GMT+08:00) 2020-07-03 18:03:07

    Real Madrid wamezindua kikosi chao cha soka ya wanawake, hatua ambayo imepongezwa pakubwa na mashabiki. Usimamizi wa Real almaarufu Los Blancos, umethibitisha kukamilisha ununuzi wa kikosi cha Tacon kwa Sh milioni 38 na kujitwalia umiliki. Klabu hiyo kwa sasa itajulikana kama Real Madrid Femenino. Katika taarifa yao, Real wamesema wamekuwa na kiu ya kuchangia vilivyo maendeleo ya soka ya wanawake ndani na nje ya Uhispania. Real ilikuwa miongoni mwa vikosi vinavyopendwa zaidi katika soka ya bara Ulaya kukosa timu ya wanawake. Fowadi Ada Hegerberg wa Olympique Lyon amesema kuundwa na hatimaye kuzinduliwa kwa Real Madrid Femenino ni hatua kubwa inayostahili kusherehekewa na wadau wa soka ya wanawake ulimwenguni kote. Kulingana naye, kikosi hicho kitafungua milango ya uchumi kwa wanasoka wengi wanaopania kujikuza kitaaluma. Hegerberg, 24, alikuwa mshindi wa kwanza wa taji la mchezaji bora duniani kwa upande wa wanawake, Ballon d'Or mnamo 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako