• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Safaricom yamteua afisa mpya wa fedha

    (GMT+08:00) 2020-07-03 18:58:38

    Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imemteua Ilanna Darcy kuwa kaimu afisa mkuu wa fedha. Darcy anachukua nafasi ya Sateesh Kamath ambaye amepatiwa nafasi nyingine kubwa zaidi. Nafasi ya afisa mkuu wa fedha ni ya pili kwa ukubwa katika kampuni hiyo na iwapo Darcy ataidhinishwa basi atakuwa mtu wa pili mwenye mamlaka zaidi kwenye kampuni hiyo. Akitangaza uteuzi huo,katibu mkuu mtendaji Peter Ndegwa amesema Darcy sasa atasimamia shughuli zote za fedha kwenye kampuni hiyo. Ilanna alijiunga na safaricom miaka mitatu iliyopita baada ya kufanya kazi na shirika la Digicel kusini mashariki ya Asia .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako