• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gharama ya usafirishaji wa maua nje yaongezeka kwa asilimia 120

    (GMT+08:00) 2020-07-03 18:59:18

    Gharama ya usarishaji wa bidhaa nje ya nchi inasemekana kuongezeka kwa asilimia 127 baada ya ndege nyingi za mizigo kusitisha oparesheni zao kwa kuofia kuenea kwa maambukizoi ya virusi vya Corona. Katibu mkuu mtendaji wa baraza la maua nchini Kenya Bw Clement Tulezi amesema kuongezeka kwa gharama hiyo huenda kukaathiri zaidi sekta ya maua nchini Kenya. Ameongeza kuwa kwa sasa ni tani 2000 tu zinazoweza kusafirishwa kwa wiki kutoka tani 3,800. Amesema hivi sasa wanategemea ndege za kubeba vifaa vya matibabu kusafirisha bidhaa zao. Kenya husafirisha maua mengi sana nje ya nchi hasa katika soko la Ulaya ambapo mwaka jana pekee wauzaji wa maua nchini Kenya walijipatia jumla ya shilingiu bilioni 120 baada ya kuuza maua nje ya nchi. Tulezi amesema hivi sasa soko la maua barani Ulaya liko wazi kwa asilimia 100 baada ya kuweka mikakati ya kuthibiti kuenea kwa virusi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako