• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya Usalama wa Taifa ya Hong Kong yaanzishwa

    (GMT+08:00) 2020-07-03 20:07:35

    Kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Sheria ya Kulinda Usalama wa Taifa ya mkoa wa Hong Kong, China, serikali ya mkoa huo wenye utawala maalumu imetangaza kuanzishwa kwa Tume ya Usalama wa Taifa ya Hong Kong, na mkuu wa mkoa huo Carrie Lam kuwa mwenyekiti wa tume hiyo.

    Lam amesema, serikali ya Hong Kong itashirikiana kwa karibu na mshauri wa mambo ya usalama wa taifa na Ofisi ya Usalama wa Taifa ya serikali kuu ya China mkoani Hong Kong, kushughulikia vizuri kazi zake, na kujitahidi kadiri iwezavyo kutekeleza sheria ya usalama wa taifa, na kulinda usalama wa taifa.

    Majukumu ya Tume ya Usalama wa Taifa ya Hong Kong ni pamoja na, kuchambua hali ya usalama wa taifa mkoani humo, kupanga kazi husika, kutunga sera za usalama wa taifa, kuhimiza ujenzi wa mfumo wa sheria na utekelezaji wa sheria wa mkoa huo, na kuratibu kazi na hatua muhimu za kulinda usalama wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako