• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Israel yashambulia vituo vya Hamas kulipiza kisasi mashambulizi ya makombora kutoka Gaza

  (GMT+08:00) 2020-07-06 09:13:09

  Jeshi la Israel jana lilisema, limeshambulia vituo vya Hamas kwenye ukanda wa Gaza, baada ya wapiganaji wa Gaza kurusha makombora matatu kusini mwa Israel.

  Kwenye taarifa, msemaji wa jeshi la Israel amesema, helikopta na ndege za kivita zilishambulia maeneo yaliyolengwa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ikiwemo "miundombinu chini ya ardhi." Hadi sasa bado hakuna ripoti iliyotolewa juu ya majeruhi.

  Kwa mujibu wa jeshi la Israel, Jumapili jioni, wanamgambo wa Palestina walirusha makombora matatu upande wa kusini mwa Israeli, na kombora moja lilizuiwa na mfumo wa Israel wa kujilinda dhidi ya makombora "Iron Dome".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako