• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Ghana watumiana salamu za pongezi kwa kutimiza miaka 60 ya uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2020-07-06 09:24:39

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Ghana Akufo Addo wametumiana salamu za pongezi kwa kutimiza miaka 60 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Kwenye salamu zake rais Xi amesema, katika miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano huo, urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili umeimarika, na ushirikiano pia umepata mafanikio makubwa, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo. Ameongeza kuwa, tangu virusi vya Corona vilipuke, China na nchi za Afrika ikiwemo Ghana zimesaidiana na kupambana kwa pamoja na virusi hivyo.

    Rais Xi pia amesisitiza kuwa anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kupenda kushirikiana na rais Addo kuzidisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, kwa kufuata pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, ili kuwanufaisha wananchi wa nchi hizo na kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.

    Kwa upande wake Rais Addo amesema, katika miaka 60 iliyopita, Ghana na China zimedumisha mawasiliano mazuri kati ya viongozi, kushirikiana kwa mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali, na kujitahidi kwa pamoja kujenga utaratibu wa kimataifa wenye amani, haki na usawa. Ameongeza kuwa, rais Xi ameonyesha uwezo mkubwa wa uongozi katika vita dhidi ya virusi vya Corona, na China imetoa misaada na uungaji mkono kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Ghana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako